Nandy – Nipo Naye Lyrics

0
Nandy Wanibariki EP Lyrics
Nandy – Wanibariki EP Lyrics

Nipo Naye Lyrics by Nandy

Asante baba kwa kuikata kiu yangu
Nimekuwa shahidi shahidi nimeuona ukuu wako
Imani haba umeitoa ndani yangu
Umekuwa mfariji mfariji tena mshauri wangu
Umerudisha tumaini langu wajua
Wanilinda kila nikipiga hatua

Tena umeondoa fedheha na mashaka yote
Pia umenitua mizigo hujaniacha mpweke
Hajaniacha, nipo naye, nipo na Yesu
Baba, nipo naye
Hajaniacha, nipo naye, nipo na Yesu
Baba, nipo naye

Naelewa fikra kuna kutabasamu na kulia
Mengi umeniepusha mengine hata sikutarajia
Pale nilipolia ulinifuta chozi na ukanishikilia
Umenitoa hatia, umenivika taji leo nafurahia

Tena umeondoa fedheha na mashaka yote
Pia umenitua mizigo hujaniacha mpweke
Hajaniacha, nipo naye, nipo na Yesu
Baba, nipo naye
Hajaniacha, nipo naye, nipo na Yesu
Baba, nipo naye

Written by; Nandy
Released date; 6 March, 2021
Album/EP; Wanibariki

 

Nandy Nipo Naye Lyrics

Leave A Reply